Baadhi ya maduka yakiwa yamewekwa chini ya ulinzi kwa kuuza bidhaa za filamu na muziki zilizoingia nchini kinyume na sheria huku baadhi zikikosa stampu ya ushuru wa bidhaa ya TRA na kukosesha serikali mapato kupitia kodi na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(wa pili kushoto) akiwasili katika soko la kariakoo jijini Dar es Salaam ambapo alifanya zoezi la kushtukiza la ukamataji wa bidhaa za filamu na muziki zilizoingizwa nchini kinyume na sheria ambapo inaikosesha serikali mapato kupitia kodi na kudumaza kazi za wasanii wazawa .Mitambo ya kuzalishia bidhaa za filamu na muziki kama zilivyokutwa katika kampuni ya Aguster kariakoo jijini Dar es Salaam katika zoezi la kushtukiza la ukamataji wa bidhaa hizo zilizoingizwa sokoni kinyume na sheria na hivyo kuikosesha serikali mapato kupitia kodi.Baadhi ya bidhaa za filamu na muziki zilizokamatwa kwa kuingizwa sokoni kinyume cha sheria kufauatia zoezi la kushtukiza la ukamataji wa bidhaa hizo ukiofanywa na Wzairi wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania, ni Baraza la Sanaa Nchini (BASATA), Chama Cha Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA) ,Taasisi ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye( kushoto) akiangalia bidhaa za filamu na muziki zilizokamatwa katika zoezi la kushtukiza la ukamataji wa bidhaa hizo katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam zilizoingizwa nchini kinyume na sheria, kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo.Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kulia)akiongea na mmoja wa wauuzaji wa bidhaa za filamu na muziki katika soko la Kariakoo , alipofanya zoezi la kushtukiza la ukamataji wa bidhaa hizo ambazo zilizoingia sokoni kinyume na sheria ,zoezi hilo lilifanywa kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania Baraza la Sanaa Nchini (BASATA), Chama Cha Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA) ,Taasisi ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Jeshi la Polisi
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Serikali imefanikwa kukamata jumla ya bidhaa za filamu na muziki 94,000 ambapo 93,529 ni za wasanii wa nje zilizoingia nchini kinyume na sheria huku bidhaa 273 za wasanii wa ndani zikiwa hazina stampu ya ushuru wa bidhaa kutoka Taasisi ya Mapato Tanzania(TRA) zikiwa ni takwimu za awali.
Hayo yamejiri kufuatia zoezi la kushtukiza lililofanywa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye leo katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuahidi kwamba zoezi hilo litafanyika nchi nzima.
Aidha aliongeza kuwa mpaka sasa takribani maduka 42 yamekaguliwa na kukamata mitambo 19 ya kufyatua kazi za wasanii (duplicators),printer 8 za Cd/Dvd,dvd writers 31,komputa 3,ups 7 kutoka kampuni ya Aguster.
“Hatua hii ni ya mwanzo kwa kuwaonyesha Watanzania kuwa agizo la Rais wa awamu ya Tano Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli la kulipa kodi na kununua bidhaa halisi kwa kutoa risiti linasimamiwa ipasavyo”, alisema Mhe. Nnauye.
Mhe.Nnauye aliongeza kuwa wauzaji wengi wa bidhaa za filamu na muziki wamekiuka sheria zinazosimamiwa na tasnia ya Filamu na muziki ikiwemo sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza na.4 ya mwka 1976 inayosimamiwa na Bodi ya Filamu Tanzania.
Waziri alizitaja sheria nyingine kuwa ni sheria ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na.23 ya mwaka 1984, Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki na.7 ya mwaka 1999 inayosimamiwa na Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki ( COSOTA) pamoja na sheria ya Ushuru wa Bidhaa sura ya 147 chini ya kanuni za stampu kwa bidhaa za Filamu na Muziki ya mwaka 2013 inayosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).
Alifafanua kuwa uchumi wa nchi na wasanii umehujumiwa sana kufuatia kuwepo kwa bidhaa za filamu zinazoingizwa nchini na kuuzwa kwa bei nafuu na kuua soko la bidhaa za ndani na kuingiza tamaduni zisizofaa katika jamii na hivyo kuchochea vitendo viovu ikiwemo ushoga.
“Bidhaa nyingi za filamu zimekuwa zikiingia nchini kwa magendo bila kulipiwa kodi na zimekuwa zikuuzwa kwa bei nafuu na hivyo kudidimiza kazi za wazawa na kuikosesha Serikali mabilioni ya fedha kupitia kodi” alisema Mhe.Nnauye.
Waziri Nnauye alitoa wito kwa Watanzania kuwa na tabia ya uzalendo kwa kukunua bidhaa za filamu zenye stampu ya TRA ili kusaidia katika kukusanya kodi na kuinua kipato cha wasanii.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. George Haule amewaomba wananchi waunge mkono jitihada za Serikali kwa kununua bidhaa za filamu zenye stampu ya TRA ili kusaidia kuongeza pato la kodi na kukomesha wale wote wanaokwepa kulipa kodi.

COOPERATIVES
A cooperative is an organised group of like-minded producers who combine to form a farmers’ group or partnership. Members share responsibilities and any profit or loss. They speak with a single voice and can purchase feed, equipment, chicks, building material and other supplies more cheaply. Eventually storage facilities can be established and a supply shop set up. The group can also have a strategic plan to reduce competition between individuals, set prices for poultry products and generally work to help one another to establish an industry on a firm footing. Trainers should provide as much assistance as possible to the farmers in establishing a working group that will spearhead the formation of a cooperative. The cooperative may eventually expand into other areas of commerce where the farmers can trade other farm produce in addition to poultry.COMMUNITY OWNERSHIP
This is similar to, but less rigid than a cooperative and is run by a committee representing a district or village community. For example, the committee may be responsible for raising point - of - lay pullets. These they sell at 17 - 18 weeks to individual egg producers and the profits are distributed amongst the community. The committee might purchase and run an incubator, and sell the chicks for meat or egg production at different ages. Or the committee may manage a small broiler or egg farm along commercial lines. In both cases there is opportunity to buy large numbers of chicks and bags of feed. This is usually attractive to the supplier and cheaper for the community. The concept of community farming is to empower people, mainly women, who have no opportunity as individual poultry keepers, to improve their circumstances and to alleviate poverty. Once formed, It can be extended to bio-security programs, vaccination programs against diseases, purchase of medical and other supplies, marketing of meat birds and eggs, dissemination of information, training programs and exchanging information, and greater opportunity to obtain micro-credit. This is critical to allow expansion of the family enterprise. There is a key role here for the poultry trainer who can assist in orchestrating the group by providing advice and guidance.BE THE FIRST TO COMMENT